Mshirika wa waziri mkuu wa Mali afungwa miaka 2 jela
30 Aprili 2024Matangazo
Tovuti ya kibinafsi nchini humo iitwayo Mali Jet ilisema kuwa hukumu hiyo dhidi ya Abdel Kader Maiga inajumuisha kusimamishwa kwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kupatikana kwa hatia ya kukashifu.
Mwanasiasa huyo alikamatwa nyumbani kwake mnamo mwezi Machi baada ya kudai tofauti kati ya Waziri Mkuu Choguel Maiga na wanachama wengine wa utawala wa kijeshi unaoongozwa na Kanali Assimi Goita.
Shughuli za kisiasa nchini Mali zimesitishwa kwa muda usiojulikana huku mwito wa kufanyika kwa uchaguzi na kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia ukiongezeka, kufuatia utawala wa kijeshi kushondwa kupanga tarehe ya uchaguzi.