1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MSUKOSUKO NDANI YA UMOJA WA ULAYA,MFUMO WA KODI WA CHAMA CHA FDP NA SHAURI LA KUFIDIA SIKU ZA KUUMWA KUTOKA LIKIZO

21 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CHNc

Gazeti la kusini mwa Ujerumani-SUDDEUTSCHE ZEITUNG lauliza: nini chanzo cha msukosuko ulioukumba hivi sasa Umoja wa Ulayxa na Ulaya ineelekea wapi baada ya kushindwa kufaulu kwa mkutano wa kilele wa Brussels ?

Gazeti laandika:

“Yule atakae kuwa na Umoja wa Ulaya unaoendeshwa barabara na kwa uwazi kabisa anabidi kubomoa taasisi za zamani tangu ndani ya umoja wenyewe hata katika nchi zanachama.Bnadala lakini ya kuchukua hatua kama hizo zinazohitajika ingawa zinaudhi,wanasiasa wa Ulaya wamekimbilia upande wa sera za katiba na nje.Jukumu la UU na jinsi ya kuuongoza usoni limepewa kisogo na mwishoe,zimefunguliwa mlango nchi kama Bulgaria na Rumania kuwa wanachama ilihali hazikuwa tayari na kuanza kuikaribisha Uturuki.”

Ila sawa na hizo za SDZ zimetolewa na STUTTGARTER ZEITUNG.Gazeti lachambua:

“Katika UU ,rais Jacques Chirac wa Ufaransa,Kanzela Schröder wa Ujerumani na Kamishna wa UU Bw.Verheugen miaka kadhaa sasa wakilenga shabaha ambazo hazilingani-yaani kuupanua uwanachama wa UU kwa kuwajumuisha wanachama wapya na wakati huo huo kuuimarisha.Wameruhusu kutoimarishwa kifedha kujipanua kihistoria kwa UU hadi Ulaya ya mashariki.Schröder na Chirac kama vipofu wamekuwa wakisonga mbele kuupanua UU.Rumania na Bulgaria zikaribishwe, halafu Uturuki na mwishoe nchi za Balkan.

Hatua hizo zote zimepangwa na kutekelezwa bila kuwashauri wananchi wa Ulaya.”-laandika Stuttgarter Zeitung.

Likitukamilishia mada hii,gazeti la DIE TAGESPOST kutoka Würzburg linahoji mchango wa Uingereza katika mabishano ya mchango wa fedha katika UU.Laandika:

“Imesadifu kuwa Uingereza itakayochukua umwenyekiti wa Umoja wa Ulaya hapo julai mosi.Waziri mkuu Blair alieyatia munda maafikiano yaliokaribia kufikiwa juu ya mpango wa fedha wa Umoja huu kwa kutetea masilahi ya kizalendo ya Uingereza,atauongoza Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha miezi 6 ijayo.Haikuwahi kutokea kwa mwenyekiti wa UU muda mfupi kabla kushika wadhifa huo kutetea dhahiri shahiri masilahi ya taifa lake mbele ya yale ya UU.Kwahivyo, Tony Blair amepoteza kila nafasi kuisemea Ulaya kwa kipindu cha nusu mwaka kama wakili wake anaestahiki.Na hata kuwa mpatanishi wa masilahi ya wanachama tofauti ndani ya Umoja huo.”

Na kwa maoni hayo ya TAGESPOST kutoka Wurzburg tunabadili mada tukigeukia mapendekezo ya chama kidogo cha FDP juu ya mfumo wa kodi:

Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung laandika:

„Mpango mpya wa mfumo wa kodi wa chama cha FDP ni kuachana na mashauri yasioingia akilini yaliotoka kabla uchaguzi ujao.sasa chama cha FDP kimeutambua ukweli wa mambo na kinaweza kutiwa maanani na mshirika wake atakeunda na chama hicho serikali baada ya uchaguzi ujao.Mpango wa chama hicho mshirika ungali ukitungwa na hivyo chama cha kiliberali cha FDP kimetaka kushawishi mkondo wake.“

Kuhusu pendekezo la mwenyekiti wa viwanda vya kazi za mikono Kentzler kuwa siku za kubakia nyumbani kwa kuumwa wafanyikazi zikatwe katika siku zao za likizo,gazeti la MÄRKISCHE ORDERZEITUNG laandika:

„Dai la Kentzler limeibuka katika wakati ambao wafanyikazi kwa kuhofia wasitimuliwe makazini ni wachache sana walioripoti wagonjwa tangu muongo mmoja kupita.Bila shaka kwa makampuni yenye watumishi wachache hilo ni tatizo kubwa, ikiwa mtumishi mara kwa mara anaripoti ni mgonjwa na haji kazini.Kwa upande mwengine hasa katika makampuni madogo, wafanyikazi wamekuwa wakijikokota kwenda makazini ingawa ni wagonjwa badala ya kujiuguza vitandani.“

Mwishoe, gazeti la WESTFÄLISCHEN NACHRICHTEN laandika:

„Kupungua mno miaka michache iliopita kiwango cha wasiokwenda makazini kwa sababu za maradhi kunakupa dhana kwamba baadhi ya wafanyikazi wakihiyari kwenda makazini ingawa wakiugua.Bila shaka hali mbaya ya kiuchumi imewafanya kuigiwa na hofu wasije wakafukuzwa kazi kwa kisingizio wakitegea tu kazi.Lakini yule kwa muda mrefu akienda kazini ilhali ni mgonjwa,anakidhuru pia kiwanda au tajiri wake,kwavile huenda akawaambukiza wafanyikazi wengine na kukilemaza kiwanda.“