Msumbiji kupiga kura Oktoba 9
1 Oktoba 2024Matangazo
Uchaguzi huo mkuu utafanyika katika wakati serikali inaendelea kukabiliana na makundi ya wapiganaji yanayofungamanishwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) katika mkoa wenye utajiri wa gesi wa Cabo-Delgado kaskazini mwa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Soma zaidi:
Miongoni mwa wagombea urais katika uchaguzi huo ni Daniel Chapo mwenye umri wa miaka 47 aliyewahi kuwa mtangazaji akisimama kwa tiketi ya chama tawala cha Frelimo.
Licha ya kutokuwa na umaarufu mkubwa katika jukwaa la siasa za Msumbiji, anatarajiwa kushinda kutokana na umaarufu wa chama chake.