1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja auawa katika maandamano ya Kenya

16 Julai 2024

Mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia maandamano mapya ya vijana wanaoshinikiza kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo William Ruto.

https://p.dw.com/p/4iNmV
Maandamano Kenya
Maandamano yaliyofanywa kote Kenya yanashinikiza uwajibikaji serikaliniPicha: TONY KARUMBA/AFP/Getty Images

Mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia maandamano mapya ya vijana wanaoshinikiza kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo William Ruto. Maandamano ya leo yameshuhudiwa kuwa makubwa.

Polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi kuwadhibiti vijana hao wanaofahamika zaidi kama GenZ. Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti maandamano katika angalau kaunti 23 kati ya 47 za Kenya.

Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu inayofadhiliwa na serikali ya Kenya imesema hadi sasa watu 50 wameuawa katika maandamano yaliyoanza mwezi uliopita ili kupinga ongezeko la ushuru na kodi.