1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muda aliopewa Trump wa kulipa dhamana umemalizika

25 Machi 2024

Muda aliopewa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump wa kutoa dhamana ya takriban dola nusu bilioni unamalizika leo (25.03.2024) Trump alipatikana na hatia ya ulaghai wa kibiashara.

https://p.dw.com/p/4e61t
Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Picha: Meg Kinnard/AP Photo/picture alliance

Kulingana na mfumo wa sheria wa mjini New York, Trump anatakiwa apeleke dola milioni 454 au atoe hati fungani za kumdhamini za kiasi hicho.

Kwa mujibu wa mahakama, rais huyo wa zamani alipandisha thamani ya mali zake kinyume cha sheria ili apewe masharti mazuri na benki.

Donald Trump na msururu wake wa mashtaka mahakamani

Hata hivyo mawakili wake wamesema Trump anaetarajiwa kukiwakilisha chama Republican katika uchaguzi ujao hana uwezo wa kutoa kiasi hicho cha dhamana.