Mazungumzo ya kuutafuta mkwamo wa kisiasa Niger yakwama
9 Agosti 2023Watawala wapya wa kijeshi wamekataa kukutana na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS.
Serikali ya kijeshi ya Niger imeendelea kukaidi shinikizo la kimataifa siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa mataifa ya ECOWAS, ambao utazungumzia uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi.
Niger yaukataa ujumbe wa upatanishi wa Umoja wa Mataifa
Uamuzi huo umezima matumaini ya mwisho yaliyokuwepo ya kuupatia mzozo huo suluhisho la kidiplomasia, na kuzua wasiwasi wa kutanuka kwa mgogoro huo kutokea taifa lenye eneo kubwa kabisa ukanda wa Sahel na lenye uzoefu wa matukio ya mapinduzi na uasi wa makundi ya Kiislamu.
Mali na Burkina Faso, ambazo pia zinaongozwa na wanasheria, hapo jana zililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzuia hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Niger, zikisema kwenye barua yao kwamba hatua kama hiyo itakuwa na matokeo mabaya na inaweza kuivunja jumuiya ya ECOWAS.