1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muhubiri ahukumiwa kifungo cha maisha jela Uingereza

Josephat Charo
30 Julai 2024

Muhubiri wa misimamo mikali Anjem Choudary leo amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuongoza kundi la kigaidi.

https://p.dw.com/p/4ivJn
Mwanaharakati wa kisiasa wa Kiislamu Anjem Choudary. Uingereza, 30/05 2014.
Mwanaharakati wa kisiasa wa Kiislamu Anjem Choudary. Uingereza, 30/05 2014. Picha: Gonzales Photo/Michael Hornbogen/PYMCA/Photoshot/picture alliance

Hukumu hiyo imetolewa siku chache baada ya muhubiri huyo kutiwa hatiani katika mahakama ya Woolwich Crown kwa kuwa mwanachama wa kundi lililopigwa marufuku lenye misimamo mikali la al-Muhajiroun, au ALM na kwa kuhamasisha uungwaji mkono wa kundi hilo. Jaji Mark Wall amesema Choudary mwenye umri wa miaka 57, anaongoza kikamilifu kundi  la kigaidi linalowatia moyo vijana kujiingiza katika vitendo vya misimamo mikali. Kundi la ALM lilipigwa marufuku na serikali ya Uingereza mnamo 2010 kama kundi linalojihusisha na kufanya, kupanga au kuendeleza ugaidi.