Mukwege ahimiza mapambano dhidi ya udhalilishaji wa ngono
3 Juni 2021Matangazo
Daktari huyo raia wa Congo ambaye ni bingwa wa upasuaji na masuala ya wanawake alikuwa amealikwa na spika wa bunge la mkoa wa Kivu Kusini kuwahutubia wabunge kuhusu suala la unyanyasaji kingono na utumiaji wa ubakaji kama silaha ya vita nchini Congo.
Mukwege alisema kujitolea kwa dhati kwa viongozi wa kisiasa katika ngazi ya majimbo na kitaifa kumekosekana katika mapambano dhidi ya machafuko mashariki mwa taifa hilo.
SOma pia: Asasi za kiraia DRC zalaani vitisho dhidi ya Mukwege
Matamshi ya Mukwege yamekuja siku moja baada ya serikali ya Congo mjini Kinshasa kuapa kuharakisha kampeni ya usalama eneo la mashariki, ambako mamia ya watu wameuliuwa na makundi ya waasi tangu mwanzoni mwa mwaka huu.