JamiiUganda
Museveni akaidi miito iliyomtaka afute sheria dhidi ya LGBTQ
1 Juni 2023Matangazo
Akizungumza katika mkutano wa maafisa wa chama chake cha NRM Museveni amesema sheria imesainiwa, na hakuna anayeweza kubadilisha mawazo yao.
Amesema kamwe chama chake hakitoi kauli tata, na kwamba kinalolisema mchana ni hilo hilo kitalirudia usiku. Wanaharakati nchini Uganda wamewataka wahisani wa kimataifa kuwawekea vikwazo viongozi wa Uganda, kwa sababu ya sheria hiyo inayochukuliwa kuwa miongoni mwa zile kali sana duniani dhidi ya ushoga.
Tangazo la pamoja la mashirika ya kutetea haki za binadamu limeilaani sheria hiyo, likiitaja kuwa ya hatari na ya kibaguzi.