1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni atetea operesheni ya majeshi yake DRC

Lubega Emmanuel8 Desemba 2021

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amelitaka baraza la usalama la Umoja Mataifa kuunga mkono hatua ya jeshi la nchi yake pamoja na lile la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwatokomeza waasi wa Allied Democratic Front - ADF.

https://p.dw.com/p/43z9Y
Afrika Uganda Edward Katumba Wamala
Picha: AFP via Getty Images

Wakati huo huo ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa nchini umetoa mwito wa kujumuishwa katika muundo wa operesheni inayoendelea sasa ili kutoa mchango wa kuwalinda raia katika operesheni hiyo.

Operesheni inayoitwa Shujaa ilianza siku kumi zilizopita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa lengo la kuwakabili waasi wa kundi la Allied Domokratic Front - ADF.

Vikosi vya Uganda vyaingia Congo vikiwasaka waasi

Operesheni hiyo ilianza siku chache baada ya visa viwili vya miripuko ya mabomu mjini Kampala ambavyo vinadaiwa kufanywa na kundi hilo la ADF.

Akikutana na mabalozi wawakilishi wa mataifa yaliyo kwenye baraza la usalama wa Umoja mataifa, rais Museveni amefafanua kuwa waliamua kuendesha operesheni hiyo baada ya kufanya mashauriano ya muda mrefu na serikali ya Congo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri MuseveniPicha: Henry Nicholls/REUTERS

Kulingana na Umoja mataifa, azma ya kufanya operesheni hiyo isichukuliwe kuwa majeshi yake ya walinda amani ya MONUSCO yameshindwa kudhibiti hali na ndiyo sababu ya Uganda na Congo kuanzisha operesheni. Ila wanataka kushirikishwa katika kuhakikisha usalama wa raia.

Ombi hilo linakuja wakati shtuma zikiendelea kwamba usalama umezorota eneo hilo tangu kuanza kwa operesheni hiyo. Kwa upande wao makamanda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaelezea kuwa operesheni itasaidia sana kukomesha mauaji ya raia wasio na hatia ambao mara kwa mara wamevamiwa na kushambuliwa na waasi wa ADF. 

Uganda yaanzisha ujenzi wa barabara DRC kuimarisha biashara

Operesheni inayoitwa Shujaa ilianza siku kumi zilizopita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa lengo la kuwakabili waasi wa kundi la Allied Domokratic Front - ADF.
Operesheni inayoitwa Shujaa ilianza siku kumi zilizopita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa lengo la kuwakabili waasi wa kundi la Allied Domokratic Front - ADF.Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la Uganda, wamepeleka wanajeshi 1,700 mashariki kwa Congo yakijumuisha vikosi vya nchi kavu na pia vile vinavyotumia zana za hali ya juu.

Rais Museveni ameahidi wajumbe wa baraza la usalama kuwa majeshi ya Uganda yataondoka Congo mara tu yakitimiza malengo yao na kuongezea kuwa hatarajii jamii ya kimataifa kuielewa vibaya Uganda kuhusiana na nia yake katika kuendesha operesheni hiyo.

Mataifa 15 ya Baraza la usalama yaliwakilishwa kwenye mkutano huo ikiwemo Marekani, China na Urusi.