1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni:Sibabaishwi na hali ngumu ya waganda

7 Juni 2022

Rais Museveni wa Uganda amesema hababaishwi na hali ngumu ya maisha inayowakumba Waganda kwani ameweka misingi bora ya kukabiliana nayo, ikiwemo wananchi wajikite katika sekta ya kilimo na kupandisha thamani mazao

https://p.dw.com/p/4CNg2
EAC Staaten Video-Konferenz | Yoweri Museveni
Picha: Philbert Rweyemamu/EAC

Ameyasema hayo kwenye hotuba yake kwa taifa hivi leo ambapo ameyahimiza mataifa ya Afrika kutambua kuwa malighafi walizo nazo zinatosha kulikwamua bara hilo kutoka katika msukosuko wa kiuchumi ambao kwa sasa unaelezewa kutokana na vita kati ya Urusi na Ukraine.

 Wanasiasa wa upinzani wamesusia kuhudhuria kikao hicho ambacho kikatiba, rais wa taifa anatakiwa kutoa taarifa kuhusu hali ya utawala wake katika kipindi cha mwaka mmoja wa fedha.

Akikariri mafanikio yake tangu alipoanzakutawala Uganda mwaka 1986, Rais Museveni ameorodhesha mikakati yake ya kuwa na mazingira endelevu ya kustawisha uchumi kupitia uzalishaji wa kilimo.

"uganda ipo kwenye mwelekeo sahihi tunachohitaji tu ni kuzingatia masuala ya mazingira" Alisema rais Museveni

 Amesisitiza kuwa maendeleo ya kijamii yatafikiwa ikiwa idadi zaidi ya watu watashiriki kilimo biashara kwa kutumia mbinu za kisasa.

 Ni kwa msingi huu ndipo ametamka kuwa hababaishwi na hali ngumu ya maisha ambapo bei za bidhaa zimepaa kwa kasi ila ni fursa kwa Uganda na mataifa ya Afrika kuzingatia kupunguza utegemezi kwa mataifa ya kigeni.

Soma pia:Museveni: Kupunguza ushuru kutavuruga mipango ya serikali

Tunahitaji kuzingatia mazingira kwani uganda imeweza kufanya kila linalowezekana kwa miaka 36 sasa" Alisema.

Aidha wakati serikali yake ikinyooshewa vidole kwa ufisadi na utumiajiholela wa fedha za umma na wapinzani na wakosoaji mbalimbali alioneza kwamba kama taifa kinachohitajika ni kuja pamoja na kupiga vita tatizo la ufisadi.

"Hakuna shida ambayo Uganda haiwezi kutatua, tuungane pamoja kupiga vita ukiritiba na ufisadi" alisisitiza katika hotuba yake ambayo ilisusiwa na wapinzani wake.

Aihimiza  Afrika kupandisha thamani mazao ya kilimo

Museveni amehimiza mataifa ya Afrika kuzidisha juhudi katika kuongeza thamani kwa malighafi za kilimo madini ili kuhakikisha kuwa utajiri wake hauhamishi na wagenikujenga uchumi katika mabara mengine.

Mfumuko wa bei za bidhaa Uganda

Akitumia mfano wa biashara zao la kahawa duniani, Museveni amelezea kuwa nchi zinazozalisha zao hilo huingiza tu dola bilioni 25 ikilinganishwa na dola bilioni 460 ambazo ndicho kiwango cha soko la kahawa duniani kila mwaka.

Soma pia:Wanaharakati Uganda wapinga washukiwa kuuawa

Wakati hu ohuo, Museveni amefichua kuwa yeye binafsi ndiye alitoa wazo kwa mwekezaji raia wa Italia kununua kahawa yote ya Uganda. Hatua hiyo imeibua mjadala mkubwa ikielezewa kuwa ukiritimba ambao unalenga kuwanyonya wazazlishaji wa zao hilo.

Wapinzani wasusia mkutano wake

Wabunge wa upinzani wamesusia kikao hicho rasmi cha hotuba kama kielelezo cha kumkosoa Musevenikwa kukataa kujitokeza na mkakati maalum wa kuwakwamua wananchi dhidi ya hali ngumu ya maisha inayowakumba  kwa sasa. Kiranja wa upinzani bungeni.

John Baptist Nambeshe amesema, hotuba ya rais Museveni haijabeba ajenda ya kuwakomboa wananchi dhidi ya changamoto ambazo mataifa mengi wanakabiliana nazo ikiwemo suala la mfumko wa bei.

"Badala ya kuleta suluhisho kama majirani zetu, Tanzania, yeye ameachia kadhia hiyo wananchi." Baptist aliiambia DW 

Kwa upande mwingine wananchi walimtarajia kiongozi wa Uganda kutangaza mikakati ya kudhibiti kasi ya mfumko wa bei za bidhaa muhimu hasa kutokana na bei ya juu ya mafuta.

Soma pia:Museven akataa mwanae kujiuzulu

Wamesema hotuba ya rahisi haijabeba suluho la kupoza machungu ya maisha ambayo wananchi wanapitia kwa hivi sasa, badala yake imebeba ajenda ambazo hazina mashiko kwa wakati huu.

Uganda | Coronavirus | Straßenhändler
mfanyabiashara mdogo mjini Kampala.Picha: Abubaker Lubowa/AA/picture alliance

wameongeza kuwa hotuba hiyo imelenga zaidi viongozi kujifikiria wao binafsi na nafasi zao serikalini, lakini mwananchi wa kawaida anaendeleea kutaabika bila serikali kuleta ahueni hata ya kupunguza bei ya mafuta.

Itakumbukwa kuwa hivi siku za karibuni Museveni aliwaambia wananchi wa taifa hilo la Afrika Mashariki kwamba hatopunguza tozo za bei ya bidhaa kutoka nje kwani itavuruga mipango ya serikali yake iliojiwekea.