Muungano unaopigania uhuru wa New-Caledonia wateua kiongozi
1 Septemba 2024Christian Tein anayezuiliwa jela nchini Ufaransa alikamatwa kufuatia maandamano ya vurugu yaliyofanyika katika jimbo hilo ambalo liko chini ya himaya ya Ufaransa katika kanda ya Pasifiki.
Christian Tein anayejiita mfungwa wa kisiaasa alikuwa miongoni mwa wanaharakati saba wanaopigania uhuru wa New-Caledonia waliopelekwa Ufaransa mwezi Juni,hatua iliyozusha vurugu mpyakatika kisiwa hicho na kusababisha vifo vya watu 11.
Kuteuliwa kwake Jana Jumamosi, kuongoza muungano wa kisoshalisti wa kupigania ukombozi-FLNKS, kunatishia kuleta utata katika juhudi za kuumaliza mgogoro wa jimbo hilo,uliosababishwa na mpango wa Ufaransa wa kutaka kuleta mageuzi ya sheria ya uchaguzi katika eneo hilo.Wakaazi asilia wa jimbo hilo wanakhofia Ufaransa inataka kuzuia malengo yao ya kupigania uhuru kamili wa jimbo lao.