1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karibu watu 19 wafa kwa maporomoko ya udongo, Indonesia

14 Aprili 2024

Karibu watu 19 wamekufa na wengine wawili hawajulikani walipo kufuatia maporomoko ya udongo katikati mwa Indonesia, zimesema mamlaka za eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4ek3t
Indonesia | Mvua kubwa | Waokoaji wanatafuta manusura
Mvua kubwa zimekuwa zikisababisha majanga katika baadhi ya maeneo nchini Indonesia. Pichani ni familia za watu waliokufa baada ya mvua kubwa kuibua mafuriko katika jimbo la Nusa Mashariki Tenngara, Indonesia, 2021Picha: Aditya Pradana Putra/Antara Foto/REUTERS

Mkuu wa idara ya majanga Sulaiman Malia amesema miili ya watu hao pamoja na manusura wawili waliondolewa usiku wa Jumamosi kwenye vijiji vilivyokumbwa na maporomoko hayo huko Tana Toraja, katika jimbo la Sulawesi Kusini.

Afisa huyo ameliambia shrika la habari la AFP hii leo kwamba, bado wanawatafuta wahanga wengine na kuongeza kuwa kuna watu wawili ambao pengine wamefukiwa na udongo.

Amesema, eneo hilo na mengine yaliyo jirani yamekumbwa na mvua kubwa, hasa wiki iliyopita na kusababisha maporomoko ya udongo katika maeneo ya makazi ya raia yaliyopo kwenye miteremko, na kufukia makazi.

Soma pia:Watu 20 wafariki katika maporomoko ya udongo China