1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano wa kibiashara waibuka kati ya Kenya na Tanzania

7 Novemba 2017

Kumezuka mvutano kati ya Kenya na Tanzania kufuatia kitendo cha kuteketezwa vifaranga 6400 vilivyoingizwa nchini Tanzania pamoja na tukio jingine la kupigwa mnada hivi karibuni ng'ombe kiasi 1325 kutoka Kenya.

https://p.dw.com/p/2nAGl

Kenya imemuita balozi wa Tanzania Nairobi kutoa maelezo kuhusiana na tukio hilo. Hata hivyo kwa mujibu wa waziri wa mifugo na Uvuvi  wa Tanzania Luhaga Joelson Mpina anasema ng'ombe waliopigwa mnada hawana mwenyewe na hatua walizozichukua zinazingatia sheria ya Tanzania. Saumu Mwasimba anazungumza na mchambuzi kutoka Tanzania Gwandumi Mwakatobe kuhusiana sakata hili, katika mahojiano yalioambatanishwa hapa chini.

 

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman