Taarifa ya kukamatwa kwa mwanablogu mashuhuri na mkosoaji mkubwa wa serikali ya Uganda Fred Lumbuye zimechochea mjadala mpya leo kuhusu uhuru wa watu wanaofanya kazi ya kuuhabarisha umma na kutoa maoni kupitia majukwaa ya kidijitali kwenye mataifa ya Afrika Mashariki. Kisa hiki kinachora taswira gani kwa watumiaji wa mitandao kwenye kanda hiyo?