Waziri wa Ujerumani Baerbock aanza ziara Afrika Magharibi
16 Julai 2024Ziara hiyo ni juhudi za kuongeza ushirikiano wa Ujerumani na mataifa ya Afrika Magharibi, ili kuzuia kuenea kwa ukosefu wa usalama kunakoshuhudiwa kwa sasa katika mataifa ya Sahel.
Soma pia: Baerbock aiangazia Sudan katika ziara yake ya Afrika Mashariki
Akizungumza mjini Dakar, Baerbock amesema usalama wa Afrika Magharibi na maendeleo ya siku zijazo ni mambo yenye uhusiano wa karibu na usalama na maendeleo ya Ulaya. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani amedai kwamba matatizo yanayoikabili Afrika magharibi kama ugaidi, uhamiaji, uhalifu na umaskini yanaiathiri pia Ulaya moja kwa moja.
Soma pia: Baerbock akutana na kiongozi wa kijeshi wa Mali
Ziara hii ya Baerbock inajiri wakati kukiwa na wimbi la ukosefu wa usalama katika eneo la Sahel. Baerbock atakuwa nchini Ivory Coast, nchi ambayo pamoja na Senegal, zinachukuliwa kama washirika wawili wakuu zaidi wa Ulaya, wakati ambapo mataifa mengi zaidi ya ukanda huo yanaigeukia Urusi kama mshirika.