1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati wa mazingira ahukumiwa miezi 16 Ujerumani

18 Julai 2024

Mahakama moja ya mjini Berlin, nchini Ujerumani imemuhukumu kifungo cha miezi 16 jela mwanaharakati wa mazingira kwa kitendo chake cha mara kwa mara cha kutumia rangi na kuweka vizuizi vya barabarani.

https://p.dw.com/p/4iRYC
Ujerumani | Kizazi cha mwisho | Maandamano katika bandari ya Mukran
Kizazi cha Mwisho (Letzte Generation) kilifunga mitaa wakati wa maandamano ya kutatiza huko Cologne, Ujerumani Machi 16, 2024.Picha: Hesham Elsherif/Anadolu/picture alliance

Taarifa ya mahakama ya Tiergarten ya katikati ya jiji la Berlin imesema mtuhumiwa huyo kutoka katika kundi la "Last Generation" amekutwa na hatia ya kuharibu mali na kukataa kutii sheria

Hata hivyo, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32 bado anayohaki ya kukata rufaa. Mahakama inamuhukumu kwa kuweka vizuizi vya barabarani katika maeneo matano tofauti kati ya Oktoba 2022 na Februari 2023.

Mtuhumiwa huyo pia hapo awali alipewa adhabu ya kulipa faini na mahakama huko Hamburg na Berlin kwa matukio kama hayo, ingawa hayakuhusishwa katika kesi hii ya sasa.