1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati wa Morocco aliyegoma kula aachiwa huru

24 Machi 2021

Mwanahistoria na mwanaharakati nchini Morroco Maati Monjib aliyekuwa jela na kugoma  kula kwa siku 19 ameachiliwa huru baada ya kushikiliwa kwa kipindi cha miezi mitatu.

https://p.dw.com/p/3r3xe
Maati Monjib | marokkanischer Historiker und Menschenrechtsaktivist
Picha: Fadel Senna/AFP

Msomi huyo mwenye umri wa miaka 60 amekaribishwa uraiani na marafiki na wafuasi wake hapo jana baada ya kuachiwa kutoka jela ya El Arjat karibu na mji wa Rabat alikokuwa akizuiliwa tangu alipokamatwa.

Monjib anayefahamika kwa msimamo wake wa kuzikosoa waziwazi mamlaka nchini Morocco alikamatwa Desemba 29 kama hatua ya uchunguzi wa awali kuhusu tuhuma za kuhusishwa na utakatishaji fedha.

Mwanaharakati huyo anasema tuhuma dhidi yake zimetengenezwa na sasa kwakuwa ameachiwa huru atapigania uhuru wa wafungwa wengine wanaoshikiliwa kutokana na mitizamo yao.

Tuhuma dhidi ya Monjib zimehusishwa na usimamizi wa kituo alichokianzisha cha kusaidia kuunga mkono uandishi habari za uchunguzi.

Waandishi habari sita na wanaharakati waliohusishwa kwenye kesi hiyo walihukumiwa kifungo cha hadi mwaka mmoja jela.Watatu wameikimbia Morocco na wamepatiwa hifadhi ya kisiasa barani Ulaya.