SiasaUingereza
Mwanamke wa Uingereza aliejiunga na IS apoteza kesi ya uraia
23 Februari 2023Matangazo
Serikali ya Uingereza ilimpokonya uraia Shamima Begum kwa misingi ya usalama wa taifa mwaka 2019, muda mfupi baada ya kupatikana katika kambi moja nchini Syria.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa Shamima Begum, mwenye umri wa miaka 23, hawezi kurejea Uingereza kutoka katika makazi yake ya sasa katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Syria. Anadai kwamba alikuwa muhanga wa "usafirishaji haramu wa watoto" wakati alipojiunga na kundi hilo.
Begum alikuwa na umri wa miaka 15 alipoondoka nyumbani kwake London mashariki kuelekea Syria na marafiki wawili wa shule mwaka 2015 na akiwa huko, aliolewa na mpiganaji wa kundi la IS.