Haki za binadamuUrusi
UN yaituhumu Urusi kwa vitendo vya mateso dhidi ya raia
11 Septemba 2023Matangazo
Alice Jill Edwards amesema kumekuwepo na madai ya kuaminika ya mateso na matendo mengine yanayokiuka haki za binaadamu yanayoendeshwa na mamlaka za urusi dhidi ya raia na mateka wa vita.
Mwangalizi huyo wa Umoja wa Mataifa alifanya ziara ya wiki moja nchini Ukraine na kuzungumza na mashuhuda waliomueleza kuwa wanajeshi wa Urusi huwatesa watu kwa kutumia shoti za umeme hadi kwenye sehemu zao za siri, kuwapiga, kuwatishia kunyongwa, kubakwa au kuuawa.
Kulingana na serikali ya Ukraine, zaidi ya visa 103,000 vya uhalifu wa kivita vimeorodheshwa.