Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika alaani ghasia za Kenya
28 Januari 2008Matangazo
ADDIS ABABA:
Mweyekiti wa Umoja wa Afrika –Alpha Oumar Konare- ametoa wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa ghasia nchini Kenya.Akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa mataifa ya Afrika- ulioanza mjini Addis Ababa, Konare ameomba kuwepo ufumbuzi wa kisiasa wa mgogoro huo. Amesema kuwa jawabu haliwezi kuwa kugawana madaraka kama kugawanya keki.Amesema hilo likifanyika kamwe amani haitapakitikana kwani daima kutakuwa na wale ambao hawatatosheka na matokeo.Hata hivyo amehimiza kuendeleza misingi ya utawala bora na pia kupigana dhidi ya ghasia.
Mkutano wa mawaziri wa Afrika unafanyika kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa muungano wa Afrika ambao utafanyika januari 29.