1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nahodha wa zamani wa Arsenal Xhaka atua Bayer Leverkusen.

7 Julai 2023

Bayer Leverkusen imemtambulisha Granit Xhaka kama mchezaji wake mpya, Nyota huyo raia wa Switzerland anarejea Ujerumani kwa mara ya pili baada ya kuondoka mwaka 2016.

https://p.dw.com/p/4TbFN
Serbien - Schweiz
Granit Xhaka, nyota mpya wa klabu ya Bayer 04 Bayerleverkusen akitokea Arsenal.Picha: Laurent Gillieron/Keystone/dpa/picture alliance

Baada ya kuwatumikia washika bunduki wa London kwa miaka saba, hatimaye kiungo Granit Xhaka amefikia tamati na kutimkia Ligi kuu ya soka Ujerumani Bundesliga.

 

Soma zaidi: Bayern na Leverkusen, nani atalitwaa taji la DFB Pokal Jumamosi?

Kupitia taarifa rasmi ya klabu, Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amemuelezea mchezaji huyo aliyewahi kuwa nahodha wa timu hiyo mwaka 2019 kwamba ''imekuwa ni safari ya aina yake na Xhaka kwake na kwetu kama klabu na kiukweli ameipambania kwa nguvu klabu yetu na anaondoka kwa heshima kubwa na tunamtakia kila la kheri katika safari yake.''

Kiungo huyo raia wa Switzerland alijiunga na Arsenal akitokea Borussia Mönchengladbach mwaka 2016 na tayari klabu ya soka ya Bayer 04 Leverkusen imemtangaza Xhaka kama mchezaji wake mpya kuelekea msimu mpya wa mwaka 2023-24.

 

Soma zaidiGuerreiro atangaza kuondoka Borussia Dortmund

Arsenal inaripotiwa kukamilisha uhamisho wa kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice kwa mkataba wa kuvunja rekodi katika ligi kuu ya Uingereza kutoka West Ham.

FIFA WM Qatar 2022 | Schweiz v Kamerun
Granit Xhaka nraia wa Switzerland anarejea tena katika ligi ya Ujerumani akijiunga na Bayer 04 Leverkusen.Picha: Lars Baron/Getty Images

Xhaka alifunga mabao 23 katika mechi 297 alizochezea The Gunners, na kuwasaidia kushinda Kombe la FA mara mbili na kumaliza katika nafasi ya pili ndani ya ligi kuu ya Premia msimu uliopita.

Katika mechi yake ya mwisho ya ligi kuu nchini akiwa na Arsenal alifunga mabao mawili katika ushindi wa 5-0 nyumbani dhidi ya Wolverhampton Wanderers.

Xhaka hapo awali alicheza kwa miaka minne katika Bundesligaakiwa Borussia Monchengladbach.

Baada ya hapo aliondoka na kujiunga na The Gunners kwa dau la pauni milioni 35 mwaka 2016 na sasa anarejea tena Ujerumani zamu hii akiwa na Bayer 04 Leverkusen.