Nairobi. Afrika kusini na Nigeria kutuma vikosi vya kulinda amani nchini Somalia.
23 Machi 2005Matangazo
Nigeria na Afrika kusini ziko tayari kutuma vikosi vyake vya jeshi katika juhudi za kulinda amani nchini Somalia.
Afisa wa ngazi ya juu nchini Kenya amesema leo kuwa nchi hizo mbili zimekubali ombi kutoka Kenya, ambayo ndio nchi serikali ya muda ya Somalia inapofanyia kazi zake, ili kusaidia juhudi za mataifa ya Afrika mashariki za kuiweka jeshi hilo la kulinda amani.