1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan ahutubia mkutano wa mabadiliko ya hali hewa jijini Nairobi

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsa

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan ameilaumu jumuiya ya kimataifa kwa ukosefu wa uongozi katika kupambana na ongezeko la joto duniani.

Bwana Annan amesema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa umoja wa mataifa juu ya hali ya hewa unaofanyika mjini Nairobi nchini kenya.

Katibu mkuu huyo amewaambia wajumbe kwenye mkutano huo kuwa ongezeko la joto ni tishio kubwa kwa binadamu.

O ton…Nchi masikini hasa katika bara la Afrika zitakabiliwa na matatizo makubwa ya uharibifu wa hali ya hewa.

Lazima tutafute mikakati ya hali ya juu ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani kwa mujibu wa malengo ya milenia.

Ametowa mwito wa kupunguza utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira kuliko kugharamia athari zake.

Pamoja na hatua zinazo tarajiwa kuchukuliwa kwenye mkutano huo ni mkakati wa kuzisaidia nchi za Afrika kujiweka sawa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hata hivyo wajumbe hawakuweza kukubaliana juu ya mpango wa kimataifa kuhusu kupunguza utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira.