1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Razak aiomba mahakama imruhusu kifungo cha nyumbani

3 Aprili 2024

Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia aliyefungwa jela Najib Razak, amewasilisha ombi mahakamani la kutaka waraka anaosema utamkubalia kuhudumia kifungo chake nyumbani.

https://p.dw.com/p/4eOmw
Malaysia | Najib Razak
Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia aliyefungwa jela Najib RazakPicha: AP Photo/picture alliance

Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia aliyefungwa jela Najib Razak, amewasilisha ombi mahakamani la kutaka waraka anaosema utamkubalia kuhudumia kifungo chake nyumbani.

Haya ni kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zinazosema kuwa Najib anaitaka mahakama iishurutishe serikali ithibitishe uwepo wa waraka huo na amri ya mahakama iliyotolewa itekelezwe. Waziri Mkuu wa zamani Malaysia akutwa na hatia

Mawakili wa waziri mkuu huyo wa zamani hawakutoa tamko kuhusiana na suala hilo. Kifungo cha Najib cha miaka 12 ambaye alifungwa jela kutokana na mashtaka ya ufisadi kilipunguzwa hadi hadi miaka 6 mwezi Februari na bodi ya msamaha iliyokuwa chini ya uenyekiti wa mfalme wa zamani wa Malaysia, Al-Sultan Abdullah Ahmad Shah. ambaye muhula wake wa miaka mitano ulifika mwisho Januari.