1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Namna China inavyowafunga Wauighur bila sababu za msingi

18 Februari 2020

Nyaraka mpya zilizovuja zinaonyesha namna mamlaka za China zinavyotumia teknolojia ya kiwango cha juu kuwafuatilia, kuwatambua na kisha kuwakamata Waislamu wa jamii ya Uighur.

https://p.dw.com/p/3Xuvz
DW Investigativ Projekt: Uiguren Umerziehungslager in China ACHTUNG SPERRFRIST 17.02.2020/17.00 Uhr MEZ
Picha: AFP/G. Baker

Nyaraka hizo zilizopatikana na DW zinatoa taarifa za kwanini watu wanakamatwa na orodha ya wale waliofungwa imeelezea hatma ya watu 311, ambao walipelekwa kwenye makambi kwasababu tu ya kufuga ndevu, kufunga au kuomba pasipoti. Wote hao walipelekwa kwenye makambi ya ufundishaji kati ya mwaka 2017 na 2018.  Mwaka 2014, mamlaka za China zilisimika mfumo wa ufuatiliaji na vituo vikubwa vya vizuzi, baada ya mripuko wa bomu la kujitoa muhanga kwenye jimbo la Xinjiang. Chama cha kikomunisti cha China kinauita mfumo huo kuwa mfumo wa hiari wa elimu ya ufundi. Nyaraka hizo zinakadiria kuwa angalau watu milioni moja wa jamii ya Uighur wanaoishi Xinjiang wamepotelea katika makambi hayo.