Nani atashinda kati ya Ronaldo, Modric na Salah?
24 Septemba 2018Kwa mara ya kwanza katika miaka 12 Messi hata hakuteuliwa kuwa miongoni mwa wachezaji watatu wa mwisho wanaowania tuzo hiyo baada ya Argentina kutolewa mapema katika Kombe la Dunia na Barcelona kubanduliwa katika robo fainali za Champions League.
Messi na Ronaldo wameshinda tuzo hiyo ya FIFA mara tano kila mmoja, na CR7 huenda akasimama mwenyewe baada ya kushinda Kombe la Champions League kwa mara ya tatu na Real Madrid kabla ya kuhamia Juventus mwezi Julai.
Kwa msimu wa sita mfululizo, Ronaldo alikuwa mfungaji bora katika Champions League akiwa na mabao 15 na pia akafunga manne katika Kombe la Dunia ikiwa ni pamoja na hat trick dhidi za Uhispania wakati Ureno ilitoka sare ya 3-3.
Luka Modric, nahodha wa Croatia alikuwa nguzo muhimu wakati waliwashangaza yengi kwa kufika fainali ya Kombe la Dunia na pia akachangia pakubwa katika ushindi wa Real Madrid wa Champions League na Kombe la Klabu Bingwa Duniani. Na kocha wake Zlatko Dalic ni mtu wa kwanza anayempigia debe "Natumai, natumai kuwa Luka Modric atakuwa mchezaji bora duniani kwa sababu anastahili. Nadhani mwaka huu alifanya kazi nzuri. Najua Messi, Ronaldo ni wachezaji wazuri sana lakini mwaka huu nadhani Luka Modric alikuwa bora katika mashindano ya Kombe la Klabu bingwa Duniani, Kombe la Dunia, Ulaya, na natumai Luka atashinda tuzo hii".
Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps anaonekana kutokuwa na uhakika lakini pia naye anaonekana kuegemea upand wa Modric "sijui, sijui….ni vigumu maana kuna wachezaji watatu ambao ni wazuri sana. Lakini kwa maoni yangu, anayestahili kushinda kati ya hao watatu ni Luka Modric. Alikuwa na msimu mzuri na Real Madrid na kushinda Champions League. Alifanya vyema katika Kombe la Dunia na kufika Fainali. Lakini sijui maana sio mimi nnayefanya uamuzi wa mwisho, lakini nilimpigia kura".
Salah amejumuishwa kwenye jukwa ahilo kwa mara ya ttau baada ya kufunga mabao 44 katika msimu mmoja akiwa na Liverpool na kuifikisha katika fainmali ya Champions League. Isipokuwa timu yake ya taifa Misri iliondolewa katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia baada za kushindwa mechi tatu.
Kocha aliyeshinda Kombe la Dunia na timu za Ufaransa Didier Deschamps anapigiwa upatu kushinda tuzo ya kocha bora mbele ya mwezake wa Croatia Zlatko Dalic na kocha wa zamani wa Real Zinedine Zidane, aliyejiuzulu baada ya kutwaa Champions League mara tatu katika miaka miwili na nusu.
Katika upande wa wanawake, mshambuliaji wa Norway anayechezea timu za Lyon Ada Hegerberg na kiungo wa Ujerumani Dzesenifer Marozsan wamejiunga na mshindi mara tano wa Brazil Marta anayechezea Orlando Pride kuwania tuzo za mchezaji bora baada ya kushinda Champions League na miamba hao wa Ufaransa.
Reynold Pedros wa Lyon, Asako Takakura wa Japan na Kocha wa Uholanzi Sarina Wiegman wanawania tuzo ya kocha borakwa wanawake.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman