1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO, Urusi wafanya luteka mkabala bahari ya Baltiki

Daniel Gakuba
14 Juni 2019

NATO inaendesha luteka za kijeshi katika bahari ya Baltiki, zinazoongozwa na kikosi namba 2 cha jeshi la majini la Marekani, maarufu enzi za vita baridi. Urusi inafanya mazoezi mkabala na hayo, katika bahari hiyo hiyo.

https://p.dw.com/p/3KTxZ
Litauen Exercise Baltic Operations | US-Soldaten bei Landung
Picha: Getty Images/AFP/P. Malukas

 

Luteka hizo za kijeshi za umoja wa kujihami wa NATO zilizopachikwa jina la Baltops 2019, zilianza tarehe 9 mwezi huu wa Juni na zitaendelea hadi tarehe 21. Mazoezi ya aina hiyo yamefanyika katika bahari hiyo kwa muda wa miaka 40 iliyopita, lakini tangu Urusi ilipoinyakua rasi ya Crimea kutoka Ukraine, NATO imejiimarisha kwenye mpaka wake wa Mashariki.

Mnamo miaka ya hivi karibuni vimetokea visa kadhaa ambapo ndege za NATO ziliingilia kati kuzizuia ndege za kivita za Urusi kuingia katika anga la nchi wanachama wa muungano huo wa kijeshi.Kikosi kilichovuma enzi za vita baridi charejeazifanya luteka za NATO za mwaka huu kuwa za aina ya kiepekee ni kwamba zinaongozwa na kikosi cha pili cha jeshi la majini la Marekani, ambacho enzi za vita baridi kilipata umaarufu kwa kushiriki katika operesheni kadhaa za kimkakati, ikiwemo ya kukizingira kisiwa cha Cuba wakati wa mzozo wa makombora baina ya Marekani na iliyokuwa Umoja wa Kisovieti.

Kikosi kilichovuma enzi za vita baridi charejea

Baltikum NATO-Manöver BALTOPS 2019 | Andrew Lewis
Andrew Lewis, kamanda wa kikosi cha majini cha Marekani kinachoongoza luteka za NATOPicha: DW/A. Prokopenko

Kikosi hicho kiliwahi kuvunjwa mwaka 2011, kwa sababu uongozi wa rais Barack Obama uliamini kwamba Urusi haikuwa kitisho tena kwa nchi za Magharibi, lakini kilirejeshwa mwaka 2018 baada ya Urusi kuimarisha shughuli zake katika bahari ya Atlantiki.

Lakini mkuu wa kikosi hicho Andrew Lewis ameiambia DW kwamba kurejeshwa kwa kikosi chake hakuilengi nchi yoyote, bali ni jibu kwa mazingira ya kiusalama yanayobadilika duniani, kutokana na kuibuka kwa washindani wapya kijeshi, hasa Urusi na China.

Luteka za Baltops 2019 zinahusisha wanajeshi 8,600 kutoka nchi 16, na nchi mbili za ukanda wa Baltiki, Sweden na Finland ambazo sio wanachama. Wanatumia manowari 50, nyambizi mbili na ndege za kivita zipatazo 40. Mazoezi yao yanajikita katika ulinzi wa anga na kujilinda dhidi ya manowari za adui.

Urusi yakaa chonjo

Symbolbild polnische Soldaten | Polen zieht Soldaten aus europäischer Eurokorps-Truppe ab
Wanajeshi wa Poland katika mazoezi hayoPicha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Kwa urusi, luteka hizi zinazofanyika katika jamhuri tatu za Baltiki za Estonia, Latvia na Lithuania ambazo zilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovieti lakini sasa ni wanachama wa NATO, zinatazamwa kwa jicho la wasiwasi.

Wakati wanajeshi wa NATO wakijizoeza kuwasili kwa meli kwenye fukwe za kisiwa cha Estonia cha Saaremaa, wale wa Urusi wanafanya luteka zao katika bahari hiyo hiyo, wakijizoeza kuzizamisha nyambizi za adui, na kuzilenga meli zake kwa makombora kutoka eneo inalolithibiti la Kaliningrad.

dw - https://p.dw.com/p/3KOGx