1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO: Uturuki iridhie uanachama wa Finland na Sweden

Hawa Bihoga
4 Novemba 2022

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ameiasa Uturuki kuweka kando kutoridhishwa kwake na juhudi za Finland na Sweden kujiunga na jumuiya hiyo ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4J3DG
Belgien NATO l Treffens der Verteidigungsminister l Stoltenberg
Picha: Kenzo Tribouillard/AFP

Katika wito wake alioutua mjini Istanbul baada ya kumaliza mkutano na waziri wa mambo ya nje Uturuki, amesisitiza majirani hao wa nchi za Nordic wamefanya vya kutosha kuhusu wasiwasi wa ankara kwa ajili ya uanachama wao.

Uturuki ambayo ilijunga na NATO mnamo 1952 bado haiko tayari kuyaidhinisha mataifa hayo baada mazungumzo kwa miezi kadhaa kwa pande zote tatu.

Kwenye madai yake serikali ya Uturuki inawataka kuwachukulia hatua kali watu binafsi inaowachukulia kama magaidi ikiwemo wafuasi wa Chama kilichoharamishwa cha Wafanyakazi wa Kurdistan na watu wanaoshukiwa kupanga mapinduzi yaliyofeli mwaka 2016 nchini Uturuki.

Soma zaidi:Urusi, China zaikosoa NATO baada ya onyo lake

Stoltenberg katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu, amesema Finland na Sweden wametekeleza ahadi yao kwa Uturuki na kuwataja kwamba wamekuwa washirika wakubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Amesema ni wakati sasa wa kuwakaribisha Finland na Sweden kamawanachama kamili wa NATO, na kujiunga kwa mataifa hayo kufanya muungano huo kuwa imara zaidi.

"Finland na Sweden zimetimiza makubaliano yao na Uturuki" amesema Stoltenberg na kuongeza kwamba Wamejitolea kwa uwazi ushirikiano wa muda mrefu na Uturuki ili kushughulikia masuala ya usalama.

Ametaja kwa huu ni wakati wa kuzikaribisha Finland na Sweden kama wanachama kamili wa NATO na kujiunga kwao kutafanya muungano wetu kuwa na nguvu zaidi na watu wetu kuwa salama."

Uturuki: Nchi hizo hazijatekeza kikamilifu mkataba

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema kuwakubalia kama wanachama wapya mataifa hayo, kutategemea na mahitaji ya taifa lake kukubaliwa na kutekelezwa kwa mkataba wa pamoja.

Tahsin Ertugruloglu - Außenminister der türkischen Nordzypern
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut CavusogluPicha: Fatih Aktas/AA/picture alliance

mkataba huo ambao ulisainiwa kabla ya mktano wa NATO wa mwezi Juniwenye vifungu 10 ambao ulipendekezwa kabla ya kikao cha NATO mwezi June, baada ya Uturuki kutishia kukutumia kura yake ya turufu.

Cavusoglu amewaambia waandishi wa habari kwamba Uturuki inaunga mkono upanuzi wa NATO lakini haiwezi kuthibitisha kwamba Finland na Sweden zimetekeleza kikamili vipengele vyote vya mkataba.

"Ni hatua muhimu kwa Uswizi kuondoa vikwazo vya silaha dhidi ya Uturuki."

Akifafanua namna ambavyo wanaona mkataba huo haujatekelezwa ipasavyo alisema

"walitathmini vema maombi ya kampuni zetu moja au mbili. Kwa upande mwingine, walikwenda kubadilisha sheria" Alisema waziri huyo wa mambo ya nje Uturuki.

"Hata hivyo, haiwezekani kusema hivi sasa kwamba nchi hizo mbili zimetekeleza kikamilifu vipengele vyote vya mkataba huo." Alisisitiza akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Soma zaidi:NATO: Urusi ni tishio la moja kwa moja kwa washirika

Finland na Sweden ziliomba uanachama wa NATO baada ya Urusi kuivamia kijeshi Ukraine mnamo Februari.

Hatua hiyo iliwalazimu kuacha sera zao muda mrefu za kutofungamana kijeshi kutokana na wasiwasi kwamba Rais  Vladimir Putin anaweza kuwavamia.

Nchi zote 30 wanachama wa NATO lazima waidhinishe itifaki ya mataifa hayo mawili ili kuwa wanachama kamili.