NATO yajitenga na kauli ya Macron ya kuingiza vikosi Ukraine
12 Machi 2024Matangazo
Stoltenberg amesema "NATO haina mpango wa kupeleka wanajeshi Ukraine, kadhalika haina mpango kujiingiza katika mzozo huo, na wala kuhusishwa washirika wake."
Stoltenberg aliongeza, hata kama ni taifa binafsi la NATO likipeleka vikosi Ukraine hatua hiyo itaathiri muungano huo kwa ujumla kwa kuwa wanachama wake wamefungwa na mkataba wa ulinzi wa pamoja.
Akifafanua baada ya kauli tata ya Macron, Stoltenberg amesema anadhani ni muhimu kwa kushauriana na kwamba wawe na namna ya pamoja ya kushughulikia masuala kwa sababu yana uzito kwa wanachama wote.