NATO yashindwa kutimiza ahadi kwa Ukraine - Stolteberg
30 Aprili 2024Akiwa kwenye mkutano wa pamoja wa waandishi habari na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine mjini Kyiv siku ya Jumatatu (Aprili 29), Stoltenberg alisema kucheleweshwa kwa misaada hiyo kunatoa fursa kwa Urusi kutumia uwezo wake dhidi ya Ukraine, wakati vikosi vya nchi hiyo vikisubiri kuwasili kwa vifaa vya kijeshi kutoka Marekani na Ulaya.
Soma zaidi: Ukraine, Urusi zaidi kudunguliana ndege zisizotumia rubani
Stoltenberg aliongeza kuwa ukosefu wa silaha kwa Ukraine umeiwezesha Urusi kusonga mbele katika uwanja wa vita na kwamba ukosefu wa mifumo ya ulinzi wa anga umeyawezesha makombora ya Urusi kulenga shabaha zake kikamilifu ndani ya ardhi ya Ukraine.
Kwa upande wake, Zelensky alisema kuwa vifaa vipya vya Magharibi vimeanza kuwasili lakini kwa kasi ya chini na akatoa wito wa kuharakishwa kwa mchakato huo.