1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO: Urusi haitoweza kutimiza malengo yake kwa Ukraine

22 Desemba 2023

Katibu Mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg anaamini kuwa Urusi "imeipoteza kabisa Ukraine" na haitoweza kutimiza malengo yake licha ya kuimarisha uwezo wake wa kijeshi tangu ilipoivamia Ukraine 2022.

https://p.dw.com/p/4aUoS
NATO-Generalsekretär Jens Stoltenberg besucht der Premierminister von Nordmazedonien Dimitar Kovacevski
Picha: Petr Stojanovski/DW

Katika mahojiano na shirika la habari la dpa, Stoltenberg ameeleza kuwa lengo la uvamizi wa Urusi lilikuwa kuizuia Ukraine kujiunga na NATO na Umoja wa Ulaya. Katibu Mkuu huyo wa jumuiya ya kujihami ya NATO amesema kukaribia kwa Ukraine kupata uanachama wa Umoja wa Ulaya ni pigo kubwa la kimkakati kwa Urusi.Stoltenberg amesema kuwa miongoni mwa gharama kubwa za vita ambazo Urusi inalipa ni uchumi wao kuyumba, kupoteza mamia ya ndege na vifaru vya kijeshi pamoja na kiasi vifo na majeruhi ya takribani watu 300,000.