Navalny alikuwa abadilishwe na mfungwa wa Kirusi Ujerumani
26 Februari 2024Washirika hao walisema muda mfupi kabla ya kifo chake, mazungumzo yalikuwa yako njiani ili kubadilishana naye na mfungwa wa Urusi aliyefungwa nchini Ujerumani, Vadim Krasikov..
Katika taarifa aliyotoa kwa njia ya vidio, Maria Pevchikh - mshirika wa Navalny anayeishi nje ya Urusi - alisema alipokea uthibitisho kwamba mazungumzo hayo yalikuwa katika awamu ya mwisho mnamo Februari 15, siku moja kabla ya Navalny kuripotiwa kufa.
Kulingana na Pevchikh, Navalny na raia wawili wa Marekani waliokuwa wamefungwa nchini Urusi walikuwa sehemu ya makubaliano hayo ya kubadilishana wafungwa.
Krasikov alikuwa anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Ujerumani kwa mauaji ya mwaka 2019 mjini Berlin ya Zelimkhan "Tornike" Khangoshvili, raia wa Georgia mwenye asili ya Chechen.
Hata hivyo, majina ya raia wa Marekani hayakutajwa.