Nchi 11 zinakutana nchini Gabon kujadili usalama
1 Desemba 2016Matangazo
Nchi 11 zinazokutana kujadili usalama katika mataifa ya Afrika ya kati, zimeutaka upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuunga mkono makubaliano yanayomruhusu Rais Joseph Kabila kuendelea kubaki madarakani baada ya muhula wake kumalizika.
Viongozi ama wawakilishi wao kutoka katika jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika ya kati ECCAS , wanakutana mjini Libreville, mji mkuu wa Gabon.
Kati ya mataifa hayo 11 yanayoshiriki katika mkutano huo uliofanyika jana, manne yanawakilishwa na viongozi wakuu wa taifa, Rais Idriss Derby Itno wa Chad, Paul Kagame wa Rwanda, Faustin-Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya kati na mwenyekiti wa mkutano huo Ali Bongo Ondimba wa Gabon.