SiasaIsrael
Suluhisho la mataifa mawili lapigiwa debe huko Barcelona
28 Novemba 2023Matangazo
Mtazamo huo umeelezwa wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa ya Ulaya na ya kiarabu uliofanyika jana mjini Barcelona nchini Uhispania.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell, amesema mataifa yote wanachama wa umoja huo pamoja na wawakilishi wa mataifa mengine karibu yote yaliyohudhuria mkutano wa Barcelona, yameafikiana juu ya umuhimu wa suluhisho la kuundwa madola mawili.
Mwanadiplomasia huyo pia amependekeza Mamlaka ya Palestina inayotawala sana eneo la Ukingo wa Magharibi ndiyo iwe na jukumu la utawala pia kwenye Ukanda wa Gaza.
Pendekezo la suluhisho la mataifa mawili linajumuisha kuundwa kwa taifa la Palestina kwenye ardhi ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza likiwa jirani na Israel.