1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoGambia

Ndege ya kikosi cha Gambia AFCON yapata hitilafu angani

11 Januari 2024

Ndege iliyoibeba timu ya soka ya taifa ya Gambia kuelekea kwenye michuano ya mataifa ya Afrika, AFCON ililazimika kutua kwa dharura leo baada kupata hitilafu kwenye mfumo wa usambazaji hewa ya Oksejeni.

https://p.dw.com/p/4b8i5
Fußball | FIFA WM Qualifikation 2026 | Gambia - Elfenbeinküste
Picha: Loveness Bernard/empics/picture alliance

Taarifa hiyo imesema ndege iliyokodiwa kwa safari ya kuelekea Ivory Coast ikiwa imekibeba kikosi cha timu ya taifa ililazimika kurejea kwenye mji mkuu wa Gambia, Banjul, dakika 10 baada ya kuruka. Marubani waligundua mfumo wa kusambaza oksijeni ulipata hitilafu.

Kampuni inayoendesha chombo hicho ya Air Cote d'Ivoire imesema inafanya uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu hiyo. Kocha wa timu hiyo Tom Saintfiet amesema wachezaji na benchi la ufundi wamenusurika kifo kwa sababu walikuwa wakivuta ya hewa hatari ya Carbon monoxide kutokana na hitilafu iliyotokea.

Kikosi hicho kilitazamiwa kuabiri ndege nyingine kwa safari ya kuelekea mjini Yamoussoukro kutakapochezwa baadhi ya mechi za michuano ya AFCON inayofungua pazia siku ya jumamosi.