Netanyahu aapa kulipa kisasi dhidi ya Wahouthi
15 Septemba 2024Netanyahu ameyasema hayo katika kikao chake cha wiki na baraza la mawaziri na amesisitiza kuwa amedhamiria kufanya kila liwezekanalo kuwarudisha kwenye makazi yao watu waliolazimika kuhama Kaskazini mwa Israel kutokana na hali ya usalama.
Soma zaidi: Jeshi la Israel lazuia kombora la masafa marefu kutoka Yemen
Netanyahu ametoa onyo hilo kwa waasi wa Kihouthi muda mfupi baada ya kundi hilo kuthibitisha kuwa ndiyo limehusika na shambulio la kombora lililofika katikati mwa Israel kwa mara ya kwanza.
Soma zaidi: Wahouthi wa Yemen waapa kulipiza kisasi shambulizi la Israel Hodeida
Hayo yanajiri wakati jeshi la Israel limekiri leo kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa shambulio lake la anga katika Ukanda wa Gaza ndilo lililowauwa mateka watatu raia wa Israel mwezi Novemba mwaka uliopita. Miili ya mateka hao ilirejeshwa nchini Israel mwezi Desemba. Kamanda wa kundi la Hamas Ahmed Ghandour, aliuawa kwenye operesheni hiyo.