Netanyahu abebeshwa lawama juu ya tukio la mkanyagano 2021
6 Machi 2024Ripoti ya tume ya uchunguzi kuhusu mkasa huo imesema kuwa waziri huyo mkuu ana wajibu wa kubainisha kwa vitendo yeye mwenyewe au kupitia utaratibu unaofanywa kwa niaba yake, masuala ambayo yanahitaji uangalizi wa ofisi yake na, ikibidi, muingilio wake, hasa katika masuala yanayohusiana na hatari kwa maisha ya binadamu.
Uchunguzi huo umegundua kwamba kuanzia mwaka 2008 hadi siku ya mkasa huo, ofisi ya Netanyahu ilikuwa imearifiwa mara kadhaa juu ya hatari zinazoweza kusababishwa na msongamano mkubwa wa watu wanaozunguka kaburi la kiongozi wa kidini wa kiyahudi Shimon Bar Yochai.
Soma pia: Netanyahu akaidi shinikizo la kimataifa
Hata hivyo waziri huyo mkuu hakuchukua hatua mwafaka kushughulikia hali hiyo.
Katika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa X, kiongozi wa upinzani Yair Lapid, amemtaka Netanyahu kujiuzulu na kuonya kuwa ni muda tu kabla ya kutokea kwa janga lingine.