1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu asema Israel iliipiga Iran, Khamenei aapa kujibu

28 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema mashambulizi ya angani ya Israel yaliiharibu mifumo ya ulinzi ya Iran na viwanda vya kutengeneza makombora.

https://p.dw.com/p/4mIJs
Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu
Netanyahu amesema mashambulizi ya Israel yaliiharibu mifumo ya ulinzi ya IranPicha: Israel's Government Press Office/XinHua/picture alliance

Netanyahu amesema katika hotuba kuwa mashambulizi hayo yaliyofanywa kote Iran, yalitimiza malengo yao yote. Mkuu wa jeshi la Israel Luteni Kanali Herzi Halevi amesema shambulizi dhidi ya Iran lilionesha majibu ambayo Israel inaweza kuyatoa dhidi ya maadui wake.

Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema nchi yake inatafakari jibu la mashambulizi hayo. Khamenei amesema shambulizi hilo, ambalo liliwauwa wanajeshi wanne na kusababisha uharibifu, halipaswi kupuuzwa au kutiwa chumvi. Naye rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema Iran haitaki vita lakini itatoa kile alichokiita jibu mwafaka.

Soma pia: Watu 45 wauawa katika mashambulizi ya Israel kaskazini mwa Gaza

Wakati huo huo, Misri imependekeza mpango wa usitishwaji mapigano kwa siku mbili ili kubadilishana mateka wa Israel na wafungwa kadhaa wa Kipalestina. Rais Abdel Fattah el-Sissi amesema usitishaji huo wa mapigano utaruhusu pia msaada wa kiutu kuingizwa Gaza.