1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano juu ya msikiti Al-Aqsa

28 Oktoba 2015

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa anapoza kauli kali ndani ya serikali yake za kuvutania msikiti wa Al-Aqsa, kiongozi wa chama cha siasa kali cha Kiislamu Raed Salah amehukumiwa kifungo cha miezi 11 Jela.

https://p.dw.com/p/1GviY
Israel Jerusalem Tempelberg
Eneo la Temple Mount, IsarelPicha: Reuters/A. Awad

Netanyahu jana alikabiliana na viongozi waliokuwa wakivutana na kwa kauli kali ndani ya serikali yake wakigombania eneo tukufu uliopo msikiti wa Al-aqsa, huku wimbi la machafuko ya Wapalestina likuwa linaendelea.

Juhudi za kupunguza mvutano zikiwa tayari zimeshasambaratika, naibu waziri wa mambo ya nje Tzipi Hotovely alizidi kuchochea hofu ya Wapalestina kwa kusema, "ndoto yake ni kuiona bendera ya Israel ikipepea " juu ya eneo hilo tukufu, ambalo ni muhimu kwa pande zote mbili Waislamu na Wayahudi.

"Tutapepea bendera ya Israel, huu ni mji mkuu wa Israel na ni eneo tukufu kwa Wayahudi," alisema Hotovely.

Hata hivyo hapohapo ofisi ya Netanyahu ilitoa taarifa na kusisitiza kwamba utaratibu uliopo sasa utabaki kuwepo. Wapalestina wataendelea kusali katika msikiti huwo, na Wayahudi wanaruhusa kuuzuru tu lakini hawana ruhusa ya kusali ndani ya Al-Aqsa.

"Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu pia ameweka wazi kuwa anatarajia viongozi wote serikalini mwake watafuata maelekezo hayo, " ofisi yake ilieleza hayo katika taarifa maalum.

Hata hivyo Wapalestina wamekuwa wakiituhumu serikali ya Israel kuwa inawaruhusu Wayahudi kusali katika eneo la mlimani -- linalo julikana na Wayahudi kama Temple Mount -- ambalo limezingirwa kwa ukuta ndani ya mji mkongwe wa Jerusalem.

Ongezeko la Wayahudi wanaozuru eneo hilo na wengine wakikutikana wanasali kisiri licha ya kuwa hawana ruhusa ya kufanya hivyo, pamoja na kauli za uchochezi za wanasiasa, vyote hivi vimechangia kuongeza mvutano baina ya Waislarel na Wapalestina.

Raed Salah ahukumiwa kifungo jela

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin NetanjahuPicha: Reuters/F. Bensch

Halikadhalika kiongozi wa tawi la kaskazini la chama cha siasa kali cha Kiislamu nchini Israel Raed Salah, amehukumiwa kifungo cha miezi 11 jela kwa mashitaka ya kuchochea vurugu katika msikiti wa Al-Aqsa

Mashataka hayo ni ya tangu mwaka 2007, lakini serikali ya Israel imetishia kulipiga marufuku kundi hilo kwa kuhusika katika wimbi la vurugu la Wapalestina la hivi karibuni lilopelekea Waisrael tisa kuuawa.

Mwezi uliopita maelfu ya familia kutoka jumuiya ya Waarabu milioni 1.2 wanaoishi Israel -- ikiwa ni asilimi 20 ya idadi jumla ya lsrael, walishiriki katika maandamano yaliyoongozwa na Salah.

Salah ana historia ya uhalifu, ikiwamo kuwekwa jela kwa makosa ya uchochezi, kumtemea mate polisi pamoja na kufadhili kundi la wanamgambo wa Kiislami la Hamas.

Mvutano ulipozuka Septemba iliyopita na idadi ya Wayahudi wanaozuru msikiti wa Al-Aqsa ilipoongezeka wakati wa likizo yao ya kidini, tawi la Salah liliwashawishi Waislamu kwenda katika eneo hilo la Al-Aqsa kuulinda msikiti huwo.

Mvutano juu ya msikiti mtukufu wa Al-Aqsa uliopelekea Waisrael tisa kuuawa, unaojumuisha mashambulizi ya visu pamoja na ufyatuaji wa risasi, unahofiwa kuwa utazusha vuguvugu la tatu la upinzani wa Kipalestina linalojulikana kama Intifada. Halikadhalika Wapalestina 58 na Muisarel wa asili ya Kiarabu mmoja waliuawa katika machafuko hayo, nusu yao wakidaiwa kuwa ni washambuliaji.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/afpe

Mhariri:Yusuf Saumu