1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Netanyahu: Hamas inatakiwa kuangamizwa kama ISIS

12 Oktoba 2023

Hamas wanatakiwa kuchukuliwa sawasawa na namna ISIS ilivyochukuliwa. Wanatakiwa kuenguliwa kabisa kwenye jamii ya kimataifa," amesema Netanyahu.

https://p.dw.com/p/4XT2J
Israel Antony Blinken und Benjamin Netanjahu
Picha: Jacquelyn Martin/Pool via REUTERS

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kuliangamiza kundi la wanamgambo la Hamas, na kuutolea wito ulimwengu kulichukulia kundi hilo sawasawa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

Netanyahu amesema hayo alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken aliyeko Israel, katika ziara inayolenga kuzuia kusambaa kwa mzozo kati ya Israel na Hamas.

"Rais Biden alikuwa sawa kabisa kwa kuliita ni uovu mtupu. Hamas ni ISIS. Na kama ISIS ilivyoangamizwa, Hamas pia wataangamizwa. Na Hamas wanatakiwa kuchukuliwa sawasawa na namna ISIS ilivyochukuliwa. Wanatakiwa kuenguliwa kabisa kwenye jamii ya kimataifa," amesema Netanyahu.

Blinken kwa upande wake amemhakikishia Netanyahu kwamba Marekani itaendelea kuwaunga mkono na anatarajiwa kujaribu kusaidia kuachiwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, ambao miongoni mwao ni Wamarekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalen Baerbock pia pia anatarajiwa kwenda Israel kesho Ijumaa.