SiasaUfaransa
Netanyahu na Macron wajadili mivutano ya Mashariki ya Kati
3 Februari 2023Matangazo
Viongozi hao wamefanya mazungumzo yaliyojikita kuzungumza kitisho cha Iran na uhasama kati ya Israel na Palestina.
Ziara hiyo ya Netanyahu ambayo imewakasirisha waungaji mkono wa Palestina ilikuwa na lengo la Israel kutafuta mshikamano na mataifa ya magharibi katikati ya wasiwasi wa kuzuka vurugu kati ya Israel na Wapalestina.
Ofisi ya rais Macron imesema kiongozi huyo amemweleza Netanyahu kuwa serikali yake iko pamoja na Israel katika vita vyake dhidi ya ugaidi na iko tayari kutoa msaada wa kufufua mazungumzo yaliyokwama kati ya Israel na Palestina.
Suala la mradi wa nyuklia wa Iran pia ilikuwa ajenda muhimu ya mazungumzo baina ya viongozi hao wawili ambapo Macron ameitaka Iran kuonesha uwazi zaidi kwenye shughuli zake za nyuklia.