1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Annan ataka kuongezwa walinda amani Congo

27 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEXO

Katika repoti iliyotolewa hapo jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imepiga hatua ya kutia moyo katika maandalizi ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwakani lakini bado hakuna wanajeshi wa kutosha wa kulinda amani nchini humo kuhakisha uchaguzi huo unafanyika vizuri.

Annan amerudia tena wito wake aliotowa kwenye repoti kama hiyo mwezi mmoja uliopita kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liongeze idadi ya wanajeshi 2,500 wa kulinda amani kutoka ile ya sasa ya wanajeshi 16,700 ili kuweka usalama katika jimbo tete la Katanga wakati wa uchaguzi huo.

Pendekezo hilo linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama ikiwemo Marekani ambayo inabeba theluthi ya gharama za shughuli hizo ikiwa ni mojawapo ya shughuli kubwa kabisa zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa.