NEW YORK. Annan azilaumu Marekani na Uingereza.
15 Aprili 2005Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan anasema Marekani na Uingereza zinatakiwa kubeba lawama kwa kuiruhusu serikali ya kiongozi wa zamanai Saddam Hussein kujipatia mabilioni ya dola kupitia biashara haramu ya mafuta. Annan, ambaye pamoja na mwanawe Kojo walikabiliwa na kashfa ya kuhusika katika mpango wa umoja wa mataifa wa mafuta kwa chakula nchini Irak, alisema wamarekani na waingereza wangeweza kukomesha wizi wa mafuta lakini hawakufanya hivyo. Mapema jana waongoza mashtaka mjini New York waliwashitaki watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa hiyo ya chakula kwa mafuta. Bilionea David Chalmers Junior, mfanyabiashara wa Bulfgaria, Ludmil Dionissiev na John Irving wa Uingereza, walifikiswa mahakamani kwa kulipa hongo kwa serikali ya Saddam.