1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: AU na UM yakubaliana kuhusu kikosi cha Darfur.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuI

Umoja wa Mataifa umekubaliana na Umoja wa Afrika kupeleka kikosi cha wanajeshi elfu ishirini na tatu wa kulinda amani katika eneo la Darfur.

Hata hivyo mashirika hayo hayajakubaliana kuhusu anayepaswa kusimamia shughuli hiyo.

Makubaliano hayo, yaliyo kwenye taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, yanatakikana yaidhinishwe na Kamati ya Amani na Usalama ya Umoja wa Afrika na pia Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo, shirika la kuetetea haki za binadamu la Amnesty International limezindua ukurasa wa mtandao unaoonyesha picha za vijiji vilivyoteketezwa katika eneo la Darfur nchini Sudan.

Shirika hilo linatarajia picha hizo zitasaidia kupunguza ukiukaji wa haki za binadamu na pia kuujulisha ulimwengu hali halisi ya eneo hilo lenye mzozo.