1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ban Ki Moon-Katibu Mkuu mpya

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD30

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 192,limemchagua waziri wa mambo ya kigeni wa Korea ya Kusini,Ban Ki Moon kuwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa.Ban alie na umri wa miaka 62, atamrithi Kofi Annan anaeondoka mwezi wa Desemba baada ya kuwa na wadhifa huo kwa miaka kumi. Serikali ya Korea ya Kusini mjini Seoul, imefurahia kuchaguliwa kwa mwananchi wake na imesema ni chemchemi ya fahari ya taifa.Wakati huo huo rais wa Ujerumani,Horst Köhler katika risala yake ya pongezi,ametoa mwito kwa Ban, kuendelea na mageuzi yaliyoanzishwa na Kofi Annan katika Umoja wa Mataifa.Ban atakuwa katibu mkuu wa nane tangu kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka 1945 na ni Muasia wa pili kushika wadhifa huo.