1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Baraza lashutumu mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa AU.

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKi

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeshutumu shambulio lililofanywa mwishoni mwa juma ambalo limesababisha vifo vya wanajeshi 10 wa jeshi la kulinda amani la mataifa ya Afrika katika jimbo la Darfur nchini Sudan. Baada ya siku mbili la mjadala , balozi wa Ghana katika umoja wa mataifa Leslie Christian , ambaye ndie mwenyekiti wa baraza hilo mwezi huu, alisoma taarifa ya kushutumu shambulio hilo ambalo linaripotiwa kuwa limefanywa na kundi la waasi. Umoja wa mataifa umedai kuwa hatua zote zitachukuliwa kuwafikisha watu waliofanya uhalifu huo mbele ya sheria.