1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Gambari auonya utawala wa Myanmar

Mohamed Dahman6 Oktoba 2007

Uingereza,Ufaransa na Marekani zimesambaza rasimu ya taarifa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yenye kutaka utawala wa kijeshi wa Myanmar kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa na kuzungumza na upinzani.

https://p.dw.com/p/C783
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Ibrahim Gambari akiwa na kiongozi wa upinzani alioko kizuizini Aung San Suu Kyi wakati alipotembelea Myanmar hivi karibuni.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Ibrahim Gambari akiwa na kiongozi wa upinzani alioko kizuizini Aung San Suu Kyi wakati alipotembelea Myanmar hivi karibuni.Picha: AP

Mjumbe wa maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Myanmar Ibrahim Gambari ameuonya utawala wa kijeshi wa nchi hiyo juu ya taathira nzito za kimataifa kutokana na ukandamizaji wao wa maandamano ya kudai demokrasia.

Gambari amesema dunia sio ile ilivyokuwa miaka 20 iliopita na hakuna nchi itakayoweza kujifanyia itakvyo kwa kupuuza kanuni ambazo zinatekelezwa na nchi zote wanachama wa jumuiya ya kimataifa kwa hiyo ni muhimu kwa uongozi wa Myanmar kutambuwa kwamba kile kinachotokea ndani ya nchi yao kinaweza kuwa na taathira mbaya ya kimataifa.

Gambari pia ameelezea matumaini fulani ya kufanyika kwa mazungumzo kati ya kiongozi wa upinzani alioko kizuizini Aung San Suu Kyi na utawala wa kijeshi.

Jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia ASEAN imeliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba ufumbuzi wa amani wa mzozo wa Myanmar lazima ujumuishe wanajeshi.

Wanaharakati wanaadamana leo hii katika miji ya Asia na kwengineko duniani kupinga hatua ya utawala wa kijeshi wa Myanmar kuvunja kwa kutumia nguvu maandamano ya upinzani ambapo watu kadhaa wameuwawa wengine kujeruhiwa na mamia kutiwa mbaroni.