1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New-York: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ameitaka Marekani,...

3 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvd
ishirikiane kwa nguvu zaidi na taasisi hiyo ya kimataifa licha ya mabishano yaliyosababishwa na vita vya Iraq.Katibu mkuu Kofi Annan ametahadharisha vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa visiwe chanzo cha kuopuuzwa haki za binadam."Pekee kwa kushirikiana na umoja wa mataifa ndipo ugaidi na vitisho vyenginevyo vitakapoweza kushindwa nguvu" amesema hayo katibu mkuu Kofi Annan katika hotuba iliyochambua muongozo wa kisiasa wa umoja wa mataifa.Marekani inazituhumu nchi tano kujaribu kutengeneza silaha za maangamizi.Viopngozi wa mjini Washington wanatishia kuzichukulia hatua nchi hizo."Yaliyojiri Iraq yanabidi kuwa funzo kwa Iran,Korea ya kaskazini,Syria,Libya na Cuba" alionya katibu wa dola katika wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani John Bolton.Ameongeza kusema "Marekani inazingatia uwezekano wa kuchukua hatua zinaziostahiki."