1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New-York: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ametoa mwito ...

16 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFs3

wa kutolewa "misaada ya kila aina kwa Burundi".Amesema misaada yote inahitajika ili kuepusha balaa la kutoweka dalili za amani zilizoanza kuchomoza nchini humo.Katika ripoti yake kwa baraza la usalama,katibu mkuu Kofi Annan ameitaja jumuia ya kimataifa iharakishe misaada iliyokwisha ahidiwa na iwe karim katika meza ya majadiliano ya washirika wa Burundi itakayofanyika mjini Brussels mapema mwakani."Matumaini ya amani yameanza kuchomoza nchini Burundi-yanaweza kufifia ikiwa hali ya maisha ya wananchi haitaimarika" ameonya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan.Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa ,watu karibu milioni moja wanahitaji misaada ya chakula na wengine zaidi ya laki moja wanakabiliwa na ukosefu wa chakula.Ripoti inasema asili mia 17 ya wanchi wa Burundi wameyahama maskani yao ,na laki sabaa kati yao wanaishi uhamishoni nchini Tanzania.Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoripuka mwaka 1993 katika nchi hiyo ndogo ya Afrika kati,vimegharimu maisha ya watu karibu laki tatu.Makubaliano ya amani yaliyotiwa saini october iliyopita mjini Pretoria yameanza kutekelezwa.